Amos 5:4-6

4 aHili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi;

5 bmsitafute Betheli,
msiende Gilgali,
msisafiri kwenda Beer-Sheba.
Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni,
na Betheli itafanywa kuwa si kitu.”
Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni, jina lingine la Betheli kwa dhihaka.


6 dMtafuteni Bwana mpate kuishi,
au atafagia nyumba ya Yusufu kama moto;
utawateketeza, nayo Betheli
haitakuwa na yeyote wa kuuzima.

Copyright information for SwhKC